Hutoa taarifa kuhusu usanifishaji mfumo tumizi katika Serikali. Usanifishaji huu unajumuisha maeneo ya utumikaji na urahisi, yanayolenga huduma, uzingatiaji wa viwango vya wazi, utumikaji tena, urahisi wa kubadilika kulingana na hali na kutumika maeneo mengine mbalimabali
Nyaraka hii ina viwango vya vikoa ili kuhakikisha upekee, kuwezesha utambuzi rahisi na kuzuia migongano ya majina kati ya taasisi za umma. Pia inaeleza kwa kina viwango vya kutaja vikoa vya kategoria tofauti za taasisi za umma serikalini.
Nyaraka hii inaelezea viwango vya utengenezaji wa mifumo ndani ya Taasisi au upatikanikanaji wa mifumo ya TEHAMA kutoka nje ya Taasisi. Inaonyesha zaidi viwango vya Uendeshaji, matengenezo na matumizi ya mifumo hiyo.
Miongozo ya Ufuasi wa Uhakiki wa Ubora kwa Mifumo Tumizi ya Serikali Mtandao inaeleza njia ambazo Taasisi za Serikali au wakaguzi/ wakadiriaji watatumia kuhakiki ufuasi wa Mifumo Tumizi ya Serikali Mtandao kwa masharti ya ubora.
Hutoa maelezo yanayohusiana na utoaji wa huduma za Serikali zilizo muhimu, nyumbufu na nyeti kwa mahitaji ya wananchi pamoja na huduma za kawaida zinazoweza kutumiwa tena na taasisi nyingine za umma.
Hufafanua maagizo ya usanifishaji wa taarifa kwa ajili ya ukusanyaji wa data, upatikanaji, umiliki, usalama na usiri, uhifadhi na utunzaji, ufafanuzi na viwango vya matumizi ya data za kawaida na metadata.
Hutoa taarifa za miundombinu ya teknolojia inayosaidia shughuli za Serikali kama vile seva, kituo cha kazi, uhifadhi na miundombinu ya mtandao, utoaji leseni wa program za kompyuta, kukabili majanga ya TEHAMA na uendelevu wa shughuli, usimamizi wa mtoa huduma za TEHAMA, vipengele vya usimamizi wa rasilimali watu na huduma.
Nyaraka hii inaelezea viwango na miongozo ya kiufundi ili kuhakikisha ufanisi na unafuu wa gharama pamoja na utayari wa miundominu ya TEHAMA katika kujenga miundombinu yoyote inayomilikiwa na serikali ikiwamo barabara & madaraja, reli na majengo.
Nyaraka hii inatoa miongozo na vigezo vya kuinua mifumo ya pamoja ya Serikali ya mtandaoni inayotegemea “Cloud” au inayosimama pekee, kama vile ofisi ya kielektroniki (eOffice), Mfumo wa Utumaji Barua pepe Serikalini (GMS), na Mfumo wa Usimamizi wa Rasilimali (ERMS).
The Technology Roadmap aims to safely yet harmoniously set a clear path towards acquiring, development, implementation, retirement and management of existing, upcoming and emerging technologies. The roadmap also provides a glimpse on near and far future technologies that the government intend to acquire, develop, use and retire in its provision of satisfactory, efficient, cost-effective and effective services.
Hutoa taarifa kwa serikali kuhusu kubadilishana, kushirikiana na kujumuisha taarifa na kupanga michakato yake kwa kutumia viwango vya wazi vya kawaida
Hutoa taarifa ya namna ya kukinga na kulinda kiiktisadi taasisi za umma kutokana na matishio ya kiusalama wakati huo huo na kufuata masharti ya kiusalama na kisheria kwa ajili ya usiri, faragha, ufikiwaji, upatikanaji na uadilifu.
Inatoa maelezo yanayohusiana na serikali nzima, huduma za serikali, data, program tumizi na modeli rejea za teknolojia zinafafanuliwa.
Miongozo hii inatoa maelekezo kuhusu namna Mwongozo wa Utendaji wa Kamati ya Uendeshaji wa TEHAMA kwa Taasisi itakavyoendeshwa kwenye sekta ya umma kwa kueleza maudhui ya waraka wa kamati unaotamka masharti ya marejeo.
Hutoa maelezo ya usanifishaji utangamanishi kwa namna kuwa program tumizi mbalimbali za taasisi za umma zinatangamanishwa kuwezesha ubadilishanaji taarifa ndani ya serikali.
Mwongozo huainisha seti ya mapendekezo ya taratibu za usimamizi ambao viwango na miongozo inayohusiana na serikali mtandao hupitia kutoka ngazi ya taifa na kuchukuliwa na kutekelezwa ngazi ya taasisi ya umma.