Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Maswali ya Jumla
Ndio nilazima taarifa za mtumishi zibadilishwe kwa kufanya yafuatayo;
Ingia kwenye mfumo wa TSMS
Nenda sehemu ya profile iliyopo kwenye kona ya juu kulia kwenye mfumo sehemu ambapo mara nyingi watumiaji hupenda kubonyeza ili kutoka nje ya mfumo (Logout).
Baada ya kubonyeza kitufe cha profile nenda kwenye edit na badilisha taarifa zako ikiwemo baruapepe kwakuweka mpya ya taasisi uliyohamia.
Kisha bonyeza kitufe cha save ili mfumo uweze kutunza taarifa mpya zilizowekwa.
Ni lazima usajiliwe kwanza kabla ya kuanza kuingia
Upande wa kushoto chini ya Menyu ya TEHAMA, chagua “Security Incident”
Jaza maeneo yote yanayotakiwa kwa mujibu wa fomu
Bofya kitufe cha “Submit” baada ya kukamilisha
Baada ya kufanikiwa kuwasilisha tukio la usalama, utapokea uthibitisho kuwa umefanikiwa kuwasilisha tukio la usalama
Kama huna akaunti ya huduma kwa mteja, tuma baruapepe kwa egov.helpdesk@ega.go.tz au piga simu +255764292299, +255763292299 kuomba akaunti. Akaunti itafunguliwa kwa watumiaji wa taasisi za umma walioidhinishwa tu. Baruapepe ya kuhakiki itatumwa na kukutaka kutayarisha na kuthibitisha nywila yako
Kama una akaunti ya huduma kwa mteja, tuma baruapepe au piga simu +255764292299, +255763292299 kueleza tatizo unalokabiliana nalo
Ni lazima ulingie/logia kwenye GISP kwa kubofya kitufe cha “login” upande a juu wa ukurasa
Ingiza utambulisho wako (jina la mtumiaji na nywila)
Upande wa kushoto kwenye Menyu ya Huduma, chagua “Requested Services”
Huduma zilizoombwa zitaonekana, halafu tafuta au chagua huduma iliyoombwa kuangalia hatua iliyofikia
Huduma na Mifumo ya Mamlaka imepanwa katika makundi yafuatayo;
Huduma za Ushauri wa Kitaalamu na Msaada wa Kiufundi
Mifumo Shirikishi ya TEHAMA
Huduma ya Kuhifadhi Mifumo (Miundombinu kama Huduma , Mfumo kama Huduma)
Utengenezaji Mfumo
Mtandao wa Mawasiliano Serikalini (GOVNET)
Huduma za Serikali kupitia Simu za Mkononi
Utafiti na Mafunzo
Bango la Matangazo
Ili uweze kujua hatua ya mradi wa TEHAMA uliowasilishwa mtumiaji anatakiwa kufanya yafuatayo;
Mtumiaji anatakiwa kuingia kwenye mfumo wa GISP
Baada ya kuingia kwenye mfumo chagua sehemu ya Register ICT Project na kufanya uchaguzi wa sehemu ya All Projects ili kuona hatua iliyofikiwa ya mapito ya mradi mpya wa TEHAMA