Tunahudumia na kuwajali Wanufaika wa mifumo na huduma zetu ambao wamegawanyika katika makundi mawili. Wanufaika hawa ni Taasisi za Umma na Wananchi. Kwa mantiki hiyo Mamlaka inatoa huduma miongoni mwa taasisi za umma (G2G) ili kuongeza na kuboresha uwezo wa kutoa huduma kwa Wananchi (G2C), Watumishi wa Umma (G2E) na Wafanyabiashara (G2B).
Kwa hiyo, Mamlaka inalenga kujenga uwezo wa Taasisi za umma kutekeleza Sera ya Serikali Mtandao, Mikakati na jitihada nyingine za Serikali mtandao na kuweka mazingira bora kwa taasisi za umma kutumia TEHAMA katika kutoa huduma bora kwa watumishi wa umma, wananchi na wafanyabiashara.