Sababu
- Mtandao unashindwa kuunganishwa kwa haraka
- Ukubwa wa jalada umzidi kiwango kinachoruhusiwa cha 20MB
Ufumbuzi
Njia ya 1
Kama tatizo linasababishwa na kasi ya uunganishaji;
- Thibitisha kama tatizo ni kasi ya mtandao kwa kufungua mitandao mingine kama vile Google, yahoo n.k. Iwapo mitandao hiyo inafunguka kwa urahisi, basi kuna tatizo kwenye mtandao wako, kwa msaada zaidi wasiliana na msimamizi wa GMS wa taasisi yako
- Kama mitandao mingine nayo haifunguki, tafuta mtandao wa intanet mbadala wa haraka. Kwa mfano tumia modem
- Ambatisha tena jalada na tatizo litakwisha
Njia ya 2
Kama Ukubwa wa jalada umezidi kiwango kinachoruhusiwa;
- Kama unatuma majalada mengi, yatume katika vikundi vidogovidogo, tatizo litakwisha
- Kama unatuma jalada moja tu linalozidi kiwango kinachoruhusiwa (20 MB), punguza jalada kulingana na ukubwa ulioruhusiwa. Tumia mifumo tumizi ya kupunguzia kama vile WinRAR au ZIP. Kama hauna mifumo hiyo, kwa msaada zaidi wasiliana na msimamizi wa GMS wa taasisi yako
- Ukikamilisha njia ya pili hapo juu, ambatisha tena jalada na tatizo litakwisha
- Kama tatizo linaendelea, kwa msaada zaidi, wasiliana na msimamizi wa GMS wa taasisi yako