emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Sababu

  1. Ama unatuma baruapepe kwa kikundi kisichoidhinishwa
  2. Kunatokea alama kama vile -,*,> n.k kwenye uga wa anwani yako (To: Cc: or Bcc :)
  3. Seva ya baruapepe imekataa kuhalalisha mpokeaji mmoja au zaidi

Ufumbuzi

  1. Logua kwa kubofya kitufe cha “logua” na logia tena. Hatua hii itatanzua tatizo lako
  2. .Kama tatizo linaendelea, kwa msaada zaidi wasiliana na msimamizi wa mfumo wa GMS katika taasisi yako.

Sababu

  1. Inawezekana unakabiliwa na tatizo la mtandao kutounganishwa kwa haraka.
  2. Kivinjari chako kinaweza kuwa kinarejea kwenye ukurasa wa wazi uliopita ambao tayari umehifadhiwa kwenye historia ya kivinjari na bado kina taarifa ileile ambayo imekwisha angaliwa kwa mara ya mwisho au imefunguliwa wakati mtandao una tatizo la kutounganishwa kwa haraka

Ufumbuzi

Njia ya 1

  1. Logua (Logout) kwa kubofya kwenye kitufe cha logua
  2. Logia (login) kwa kutumia kivinjari tofauti kwa mfano. Google Chrome, Mozilla Firefox etc.
  3. Tafuta intaneti mbadala ya haraka kwa mfano unaweza kutumia modem na kulogia tena. Ukimaliza kuingiza jina na nywila ya mtumiaji, kivinjari kitabaini uunganishaji wa intaneti haraka na uga wa modi utaonesha otomatiki na bila shaka na ukurasa husika utafunguka na kuonesha michoro yote iliyowasilishwa.

Njia ya 2

  1. Kama huna suluhisho mbadala, logia tena kwa kuingiza jina na nywila na bofya logia. Lakini kama ukurasa husika unafunguka na baruapepe zilezile zilizopangwa bila michoro, logua tena na ingiza jina la mtumiaji na nywila na kwenye uga wa modi chagua otomatiki halafu bofya kitufe cha logia.
  2. Ukurasa wako utafunguka ukiwa na baruapepe zilizopangwa vizuri na michoro yote; kama bado, logua tena kwa kubofya kitufe cha logua

Njia ya 3

  1. Logia tena kwa kuingiza jina la mtumiaji na nywila, na kwenye uga wa modi chagua otomatiki na utapata ukurasa wenye baruapepe zilizopangwa vizuri na michoro yote, kama haitatokea hivyo, kivinjari chako kitakuwa kimechukua taarifa za logia kutoka kwenye data zake
  2. Kutanzua tatizo hili, wasiliana na msimamizi wako wa mfumo wa GMS wa taasisi yako ili akusaidie kushughulikia historia ya kivinjari (majalada yaliyoingia) halafu jaribu logia tena.

Zingatia: Iwapo baada ya jitihada zote hizo zilizotajwa hapo juu na bado GMS inafunguka na baruapepe zisizo na michoro, USIWE NA WASIWASI. Hili ni tatizo dogo ambalo hujitokeza wakati dirisha linapofunguka/ na kuonekana hivyo wakati mtumiaji anapojaribu kulogia kwenye GMS wakati akiwa na intaneti wakati wa uunganishaji wake unapokuwa chini. Itafunguka kama kawaida na michoro yote wakati intaneti itakapotulia/kuwa na kasi