emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

WACHAMBUZI WA MIFUMO YA TEHAMA WAJENGEWA UWEZO


WACHAMBUZI WA MIFUMO YA TEHAMA WAJENGEWA UWEZO


Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA), imeandaa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo Wachambuzi wa Mifumo ya TEHAMA wa taasisi mbalimbali za umma.

Mafunzo hayo ya siku 5 yanatolewa na kampuni ya kimataifa ya Koenig Solutions, yanalenga kuwajengea uwezo maafisa hao katika sekta ya ujenzi na uchambuzi wa mifumo ya TEHAMA katika taasisi zao.

Katika mafunzo hayo yanayoendelea Kibaha mkoani Pwani, pia yameshirikisha maafisa kutoka baadhi ya Taasisi za Serikali ikiwemo e-GA, Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Wizara ya Ardhi, pamoja na Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuongeza maarifa katika kuwahudumia wananchi.