emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

RAIS WA ZAMBIA ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA e-GA


RAIS WA ZAMBIA ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA e-GA


Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema, ametembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wakati wa Mkutano wa Serikali Dijitali Afrika (Africa Digital Government Conference), unaofanyika katika jiji la Lusaka nchini humo.

Mhe. Hakainde amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Lt. Gen. Mathew Edward Mkingule,na kuona mifumo mbalimbali ya kielekroniki iliyojengwa na kusanifiwa na e-GA ukiwemo mfumo wa Ofisi Mtandao (e-Office), Mfumo wa Usimamizi wa Shughuli za Taasisi (ERMS), Mfumo wa Baruapepe Serikali (GMS).

Mkutano huo ni jukwaa muhimu linaloangazia matumizi ya teknolojia katika kuboresha utendaji wa serikali barani Afrika. Katika mkutano huo, wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa serikali, wataalamu wa teknolojia, na washirika wa maendeleo, hukutana ili kujadili mikakati ya kuboresha mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi.