emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

MAAFISA HABARI,UHUSIANO NA MAWASILIANO WA SERIKALI WATAKIWA KUTUMIA MIFUMO


MAAFISA HABARI,UHUSIANO NA MAWASILIANO WA SERIKALI WATAKIWA KUTUMIA MIFUMO


Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali, wametakiwa kutumia mifumo ya Serikali katika mawasiiano, ili kulinda usalama na usiri wa taarifa za Serikali.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Huduma za TEHAMA wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bw. Ricco Boma, wakati akichangia mada kuhusu mabadiliko ya teknolojia katika mawasiliano, kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika mkoani Morogoro.

Amesema, katika ulimwengu wa sasa taarifa ni mali, hivyo Maafisa Habari ambao ndio wenye jukumu la kuhabarisha umma, wanapaswa kuzilinda taarifa za Serikali kwa kutumia mifumo mbalimbali ya Serikali katika Mawasiliano

Aidha ameongeza kuwa, matumizi ya TEHAMA katika mawasiliano yana faida nyingi ikiwa ni pamoja na habari kuwafika wananchi kwa wakati.

"Pia, kupitia mifumo ya TEHAMA, wananchi wanaweza kutoa maoni, ushauri, malalmiko au pongezi kwa Serikali kwa njia rahisi na kupata mrejesho kwa wakati kupitia mfumo wa e- Mrejesho.

Mfumo wa e-Mrejesho umetengezwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa, kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)