emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

FAHAMU KUHUSU eBarua


FAHAMU KUHUSU eBarua


HAKUNA mtandao!!!?, hakuna tatizo kazi iendelee! Hii ndiyo kauli unayoweza kusema ukiwa unatumia toleo jipya la baruapepe za serikali (GMS Client) ambayo inachagizwa na jina jipya la e-Barua.

Mfumo huu uliobuniwa na kusanifiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao umeingia katika maboresho muhimu katika kujibu changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa watumiaji wake ambao ni watumishi ndani ya wizara,halmashauri na taasisi za Umma.

Moja ya changamoto iliyopatiwa majibu katika toleo hili jipya,ni uwezo wa mtumiaji kusoma na kutumia barua pepe zake bila kuwa na mtandao wa intaneti(offline mode), hii ni hatua kubwa katika mapinduzi ya serikali mtandao nchini.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kituo cha Utafiti,Ubunifu,Mafunzo na Maendeleo ya Serikali Mtandao Dkt.Jaha Mvulla amesema maboresho katika mfumo wa barua pepe za serikali yamefanyika ili kurahisha utendaji kazi na kuboresha huduma kwa wananchi.

Dkt.Mvulla amesema maboresho yaliyofanyika katika mfumo wa barua pepe za serikali yamepelekea kuzaliwa kwa nadharia ya e-Barua ambayo ni suluhu kwa baadhi ya changamoto zilizokuwa zinajitokeza huko nyuma katika baruapepe za serikali.

“Moja ya changamoto ilikuwa ni mtumishi kushindwa kusoma tena email (baruapepe) zake ambazo tayari alishazifungua lakini anataka kupitia upya ujumbe uliondikwa, kwa mfumo wa baruapepe za kawaida hauwezi kuzifungua,ni lazima uwe na mtandao,lakini mfumo wa e-Barua utaweza kuzisoma hata usipokuwa na mtandao.” Amefafanua Dkt.Mvulla.

Pia,Dkt.Mvulla ameongeza kwamba watumiaji wa e-Barua wataweza kutuma baruapepe hata wakiwa katika mazingira ambayo hayana mtandao kabisa na ujumbe huo utahifadhiwa,na kifaa chake kitakapokuwa kwenye eneo lenye mtandao barua pepe hiyo itaenda kwa mtumiwaji.

“Hapo awali kama hauna mtandao hatukuweza fanya chochote kwenye barua pepe za serikali,lakini kupitia mfumo wa e-barua utaweza kuendelea kufanya kazi popote ulipo kwa sababu utakuwa na uwezo wa kuingia ndani ya kikasha chako cha kutuma na kusoma barua pepe.” Ameongeza Dkt. Mvulla.

Sanjali na hilo,Meneja huyo ameeleza kwamba e-Barua imeanza kufanya kazi kwa majaribio (pilot) katika matoleo mbali ikiwemo kwenye programu tumizi za simu (mobile application) pamoja na toleo la kompyuta za mezani (desktop).

Pamoja na sifa hizo kuu,Dkt.Mvulla ameeleza kwamba mfumo wa e-Barua una uwezo wa kutuma taarifa (notification) kwa mtumiaji kuhusu kuingia kwa ujumbe mpya katika anuani yake ya baruapepe.

“Kutumia mfumo huu pia unaweza ukapanga baruapepe yake itumwe muda gani,hivyo utaandika na kupanga muda wako na itajituma muda ukifika Kwenda kwa mlengwa.

Kwa upande wa usalama wa mfumo huu,viwango vya kimataifa katika kulinda faragha za mtumiaji za kazi zake akiwa mkondoni vimezingatiwa.hivyo katika mfumo wa e-Barua mtumiaji hatotumia tena nywila ili kuingia kwenye mfumo.

Mfumo wa e-Barua utatumia zaidi alama za kibayometriki (alama za vidole na utambuzi wa sura ) ili kuweza kufungua na kutumia mfumo huu wa kisasa zaidi katika historia ya serikali mtandao nchini.

Kwa mujibu wa Bw.Darwin King’ani Afisa TEHAMA e-GA amebainisha kwamba hatua hiyo itaimarisha ulinzi kwa mtumiaji kwa kiwango cha juu zaidi.

“Ili e-Barua ifunguke ni lazima itambue alama zako za vidole au sura,tofauti na mfumo wa zamani ambao ulikuwa unatumia nywila ambayo mtu mwingine anaweza inakiri au ikariri kisha akatumia kuingia na kufanya mawasiliano kinyume na matakwa au ridhaa ya mhusika.” Amefafanua Bw.King’ani.

Mtaalamu huyo wa TEHAMA amebainisha kwamba katika hatua za awali za maendeleo ya ubunifu ya mfumo huu kila mtumiaji atatakiwa kuwa na simu ya mkononi yenye uwezo wa kutambua alama za kibailojia yaani ‘biometric’ ambapo baada ya kujisajili ndiyo ataweza pia kujiunga na kompyuta ya mezani.