emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

e-GA YATOA ELIMU KWA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI


e-GA YATOA ELIMU KWA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI


Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imetoa elimu kuhusu Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa Kamati tendaji ya TEHAMA ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Lengo la mafunzo hayo ni kuijengea uwezo kamati hiyo juu ya namna inavyoweza kutekeleza ujenzi wa Serikali ya Kidijiti katika taasisi hiyo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw.Ramadhani Kailima amesema kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya Maandalizi ya INEC kuelekea uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

"Nawapongeza sana Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kutujengea uwezo, maafisa wametupitisha katika maeneo ya sheria na usalama wa mifumo yetu." ameeleza Bw.Kailima.

Uwepo wa Kamati tendaji ya TEHAMA katika kila taasisi ni takwa la Kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 18 cha sheria hiyo.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika kuanzia leo jijini Dodoma