emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

e-GA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA KIMATAIFA YA VIZIWI


e-GA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA KIMATAIFA YA VIZIWI


Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imeshiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Viziwi 2024, ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Shinyanga.

Katika maadhimisho hayo, e-GA imetoa elimu kwa kundi hilo kuhusu matumizi ya Serikali Mtandao na namna inavyoweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za Serikali kwa watu wenye mahitaji maalumu.

Moja ya mfumo uliowasilishwa ni Mfumo wa Huduma za Serikali kupitia Simu ya Mkononi (mGov), ambapo Mwananchi anaweza kupata huduma mbalimbali za Serikali kupitia namba ya msimbo *152*00#.