emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Ununuzi kwa njia ya mtandao kuanza hivi karibuni


Ununuzi  kwa njia ya mtandao kuanza hivi karibuni


Serikali imemuagiza mkandarasi anayetengeneza mfumo wa ununuzi wa pamoja wa Taifa kwa njia ya mtandao nchini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kuhakikisha kuwa mradi huo unatimiza viwango vinavyotakiwa, Jarida la Ununuzi Tanzania (TPJ) limebaini.

Akizungumza wakati wa Sherehe za kutia saini mkataba jijini Dar es Salaam hivi karibuni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema mfumo huo unatarajia kuongeza ufanisi katika ununuzi wa Umma.

Upatikanaji wa Mfumo huo umepokewa kwa shauku kubwa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi (PPRA) Dr. Laurent Shirima ambaye amesema ni hatua muhimu ya kuelekea katika kuongeza thamani ya fedha ya ununuzi wa umma nchini.

Mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao utapunguza haja ya kuwasiliana ana kwa  ana na wazabuni na taasisi zinazohitaji huduma, pia utasaidia kuhakikisha ushiriki sawa na mpana wa Wazabuni na hivyo kupunguza mianya ya rushwa.

Kwa mujibu wa Kampuni ya European Dynamics iliyoshinda zabuni ya kutengeneza na kujaribu mfumo huo itakamilisha mradi  katika muda wa miezi 11 kuanzi mwezi huu.