Utekelezaji wa Serikali Mtandao ni moja ya sehemu muhimu ya maboresho yaliyofanyika katika Utumishi wa Umma, ambao umesaidia kurahisisha utoaji wa huduma zinazopatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Utekelezaji wa Serikali Mtandao umejikita katika kuboresha utoaji wa huduma miongoni mwa taasisi za umma (Government to Government), kati ya taasisi za umma na wananchi (Government to Citizens), kati ya taasisi za umma na sekta ya Biashara (Government to Business), na kwa Serikali kuwahudumia watumishi (Government to Employees).