Maofisa Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika semina ya jinsi ya kutengeneza taarifa na namna ya kuzipandisha katika Tovuti Kuu ya Serikali. Semina hiyo ilifanyika mjini Bagamoyo ambapo Mkufunzi wa mafunzo hayo aliwaasa Wakurufunzi wote kujitoa kwa dhati kupitia Tovuti Kuu ya Serikali na kuweka taarifa mpya mara kwa mara kwani wananchi wanapenda kuona taarifa mpya kila wakati.