emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Jopo la Waamuzi latembelea Wakala


Jopo la Waamuzi latembelea Wakala


Jopo la waamuzi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma limefanya kikao cha kufanya tathmini ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala kwa ajili ya Mashindano ya wiki ya utumishi wa Umma inayotarajia kuanza Juni 16, 2015 katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Jopo hilo linaloundwa na Bi. Rukia Hussein pamoja na Bi. Leila Mavika limefanya kikao hicho katika ukumbi wa mikutano wa Wakala Juni 3, 2015.

Akitaja nafasi za kinyang’anyiro hicho, Jaji Rukia Hussein amesema taaasisi za Umma zitashindana katika vipengele vitano ambavyo ni tuzo ya Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali inayoendeshwa vizuri, tuzo ya banda bora, Afua za VVU/UKIMWI katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali, tuzo ya program bora ya Uwezeshaji wa wanawake pamoja na Ubunifu katika utoaji wa huduma.

Katika kipengele cha Ubunifu, Mkurugenzi wa Biashara na Huduma SSP. Ibrahim Mahumi amesema Wakala imekuwa ikibuni mifumo mingi inawezesha taasisi za Umma kutoa huduma kwa Umma na kutoa taarifa muhimu zinazohitajika na wananchi kutoka Serikalini.

“Wakala imetumia wataalamu wake wa ndani kutengeneza Tovuti kuu ya Serikali kwa ambayo ni dirisha moja linalotoa huduma kwa Umma ambapo vipo vipengele mbalimbali vilivyoainishwa kwenye tovuti hiyo ikiwemo sekta, biashara, mambo ya nje na Serikali. Vilevile Wakala imebuni Tovuti kuu ya Ajira inamrahisishia muombaji wa ajira kuweka maelezo binafsi na kujiunga na huduma ya simu ya mkononi, pindi nafasi ya kazi inapopatikana atapata ujumbe mfupi kupitia simu yake”, alisema SSP. Mahumi.

Naye Bi. Fatma Mgembe ambaye ni “Principal ICT Officer” kutoka Kitengo cha “ICT Management Services” amesema Wakala ina huduma ya simu za mkononi ambayo hadi sasa taasisi za Serikali takriban 10 zinatumia huduma hiyo ambayo gharama kwa ujumbe mmoja ni shilingi 19 ukilnganisha na bei inayotumiwa na mitandao mingine ya simu, hii imeipunguzia Serikali gharama kwa taasisi zake.

Aidha majaji hao walitaka kufahamu namna Wakala inavyoweza kushughulikia malalamiko ambapo Meneja wa Mawasiliano wa Wakala Bi. Suzan Mshakangoto amesema Wakala ina mfumo wa huduma kwa mteja ambapo wateja wanayo fursa ya kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya mtandao na kupatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Naye Afisa Utawala Bw. Hamadi Badi aliongeza kuwa, Wakala imeweka sanduku la maoni ambalo mteja anaweza kulitumia kuwasilisha malalamiko yanayohusu huduma zinazotolewa na Wakala ili kuweza kuboresha huduma hizo.    

Wiki ya utumishi wa Umma hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata ufafanuzi wa kina wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali na Taasisi mbalimbali za Serikali zinashindanishwa lengo likiwa ni kuweza kubiresha huduma hizo kwa wananchi.