Maafisa Tehama na Mawasiliano kutoka Mikoa 5 na halmashauri 30 za kanda ya ziwa inayojumuisha Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga na Simiyu wametakiwa kutumia njia za haraka na za kisasa katika mawasiliano ikiwemo matumizi ya tovuti na mitandao ya kijamii ili kutangaza shughuli na mafanikio ya Serikali kwa umma.
Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas wakati wa uzinduzi wa tovuti za Mikoa na halmashauri zilizotengenezwa kutokana na Mfumo mpya wa Kutengeneza tovuti.
Aidha Dkt. Abbas alisema uzinduzi wa tovuti katika mikoa na halmshauri hizo ni kigezo muhimu kitakachotumiwa na Serikali katika kupima wa utendaji kazi wa Maafisa Habari katika kushughulikia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Dkt. Abbas aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa tovuti za mikoa na halmashauri za Wilaya nchini zinaendelea kuwa hai na zenye taarifa zilizozingatia muda na wakati na hilo litawezekana iwapo Maafisa Habari watatimiza malengo wanayopaswa kujiwekea katika maeneo yao ya kazi.
“Litakuwa si jambo jema kama baada ya muda mfupi tovuti hizi zinakufa kwa kubalki bila kuhuishwa. Kwa hiyo kila mmoja kwa nafasi yake hana budi kuhakikisha kuwa tovuti hizi zinahuishwa mara kwa mara ili kutambua mchango endelevu wa Serikali na wafadhili.” alisema Dkt. Abbas.
Dkt. Abbas alisema pamoja na kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya habari vinavyotumika kufikisha taarifa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na magazeti na redio, bado tovuti na mitandao mitandao ya kijamii imendelea kutumiwa na wananchi walio wengi zaidi.
“Kwa mujibu wa takwimu ziliztolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania hivi sasa Watanzania zaidi ya Milioni 19 wapo mtandaoni.” alisema Dkt. Abbas.
Naye Mkurugenzi wa Miundombinu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Bw. Benjamin Dotto alisema Maafisa Habari na TEHAMA kuwa wabunifu, wavumbuzi na siku zote kujibidisha katika kuongeza viwango vya utendaji.
“Nimatumaini yangu kuwa baada ya kutumia framework hiyo mtatoa maoni ili kuiboresha zaidi” Vilevile, wataalamu wetu wametoa technical na user manual za jinsi ya kutumia Framework hiyo, hivyo manual hizo zitumike ili pale inaletwa taarifa ya kushindwa kufanya jambo inakuwa na mantiki zaidi” Alisema Bw. Dotto.
Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 13-20 Februari, yalifadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kupitia Mradi wa PS3 na kusimamiwa na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA).