Bohari ya Dawa (MSD) ipo tayari kutumia huduma zinazotolewa na Wakala ya Serikali Mtandao ili kuboresha huduma wanazozitoa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka MSD, Bw. Isaya Mzoro katika kikao cha pamoja kati ya Wakala na Menejimenti ya MSD kilichofanyika katika ofisi za Bohari hiyo Mei 13, 2015.
Akizitaja huduma hizo, Bw. Mzoro alisema MSD itatumia huduma ya simu za mkononi pamoja na “Disaster Recovery” katika utoaji wa huduma zao.
“Tunayo Disaster Recovery sehemu nyingine lakini inatugharimu fedha nyingi kwa kuwa ni ghali na hatupati matokeo tuliyoyarajia, tunadhani ni vema tukiileta eGA”, alisema Bw. Mzoro.
Wakala ya Serikali Mtandao inafanya vikao na Menejimenti za taasisi mbalimbali za umma ili kuweza kuitangaza Wakala pamoja na huduma zake.