emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

DFID yafurahishwa na Mfumo wa Takwimu huria nchini


DFID yafurahishwa na Mfumo wa Takwimu huria nchini


Ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa  (DFID) umefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na  serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia katika utekelezaji wa uanzishaji wa mfumo wa takwimu huria nchini.

 Ujumbe huo ukiongowa na Bw. Ian Attfield akiongozana na Bi. Morag Patrick pamoja na Bw. Yisambi Mwanshemele walikutana na Mtendaji Mkuu wa Wakala ,Dkt Jabiri Bakari,  na kutathimini  jitihada  hizo  katika ofisi za Wakala tarehe 12 Machi 2015

Akizungumza na ujumbe huo, Dkt Bakari alisema jitihada za Benki ya Dunia zimesaidia katika kujenga uelewa wa jinsi mfumo wa Takwimu huria unavyofanya kazi.

Aidha Benki ya Dunia imekuwa ikitoa Mafunzo mbalimbali yaliyohusu utengenezaji wa tovuti ya takwimu huria.  Mafunzo hayo yaliwajengea uwezo watumishi wa Wakala kutengeneza  Tovuti hiyo bila kuhusisha mkandarasi

Dkt Bakari aliongeza  katika utekelezaji wa jitihada hizo, Serikali imetoa Waraka unaosimamia utekelezaji wa mfumo huo nchini, Imetengeneza Tovuti Kuu ya Takwimu Huria  (www.opendata.go.tz) ambayo inatoa takwimu za Serikali kwa Wananchi katika dirisha moja.

  “Kwa sasani takwimu za Elimu, maji na afya ndio zilizowekwa katika tovuti hiyo kulingana na Waraka wa usimamizi wa mfumo wa takwimu huria”. Alisema Dkt Bakari

Vile vile, Katika kurahisisha upatikanaji wa takwimu hizo, Dkt Bakari alisema takwimu hizo zitapatikana kwa njia ya simu za mkononi.

 Ujumbe huo ulipendekeza  kuwa Tovuti hiyo inaweza kuonyesha takwimu za misaada mbalimbali ya washirika wa maendeleo inavyotolewa na inalenga maeneo gani.