emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Mkutano wa Wadau kutoka MDAs


Mkutano wa Wadau kutoka MDAs


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu amewataka Maofisa Waandamizi wa TEHAMA kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali kuiwezesha Serikali kutoa huduma kwa umma kwa njia ya simu za mkononi na kuongeza mapato Serikalini .

Mkwizu ameyasema hayo wakati wa Kikao cha siku moja cha wadau cha kujadili huduma zitakazotolewa na Serikali kwa njia ya Simu za Mkononi (Government Mobile Services) kilichofanyika katika hoteli ya Giraffe Mjini Dar es Salaam tarehe 23 Februari 2015

“Sina shaka kuwa washiriki mna weledi mkubwa katika eneo hili ili kujadiliana kwa kina na kuwa na uelewa wa pamoja juu ya suala hili”. Alisema Bw. Mkwizu

Aliongeza kuwa majadiliano hayo yanatakiwa kuzingatia kuwa asilimia kubwa ya wananchi wetu wanaishi maeneo ya vijijini hivyo hatuna budi kubuni njia rahisi na za gharama nafuu za kuwafikishia huduma.

Akitoa shukurani kwa Mgeni rasmi, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari alisema maoni hayo yatachukuliwa kwa umakini na kwa mtazamo mpana zaidi ili yatumike katika utekelezaji wa utoaji wa huduma zilizopendekezwa