emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Wataalam wa TEHAMA nchini tanzania wahimizwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi


Wataalam wa TEHAMA nchini tanzania wahimizwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi


Serikali imewataka watalaam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) walio katika utumishi wa umma kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, weledi na ubunifu ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za serikali kwa urahisi kwa njia ya mtandao.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Hab Mkwizu alipofungua Mkutano wa kwanza wa Mwaka wa Serikali Mtandao wa Maofisa TEHAMA,Habari,Mipango na Utawala kutoka katika Wizara, Idara,Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali jijini Arusha.

"Utumishi wa umma imara hujenga serikali na Taifa imara, utumishi wa kufanya kazi kwa mazoea na kusukumwa hauna tija kwa taifa letu" Alisema Mkwizu.

Mkwizu aliongezea kwa kusema Ili serikali iweze kutimiza na kufikia malengo yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi na kupunguza malalamiko ni lazima watumishi wa umma wawajibike ipasavyo.

Halikadhalika Mkwizu alioongezea kwa kusema Serikali kwa kutambua mchango wa TEHAMA inaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zikiwemo za baadhi ya mifumo kutokuongea, kutowasiliana na kutobadilishana taarifa kati ya taasisi na taasisi pia rudufu ya mifumo ambapo kila taasisi inakuwa na juhudi za kipekee katika kusimika na kutumia miundombinu ya TEHAMA ambayo ingeweza kutumiwa na zaidi ya taasisi moja pamoja na changamoto ya mifumo kuwa na viwango vya usimikaji tofauti.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao  Dkt. Jabiri Bakari awali akiwakaribisha Wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano waliohudhuria Kongamano hilo alisema katika kuimarisha uwazi na upatikanaji wa Takwimu huria, Serikali ikishikikiana na Wakala imeendelea kuboresha miundombinu ya TEHAMA  ili  kuwawezesha wananchi kupata huduma zinazotolewa na Taasisisi mbalimbali za Serikali kwa njia ya mtandao.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya vizuri katika kufanikisha lengo kubwa la kufikisha huduma kwa wananchi na kuongeza kuwa mpango wa  Serikali uliopo sasa ni kuwa na mfumo mmoja utakaowezesha taarifa zote za wananchi kuwa katika sehemu moja.

Dkt.Jabiri aliongeza kwakusema kuwa washiriki zaidi ya 500 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali wamepata fursa ya kujadili  masuala mbalimbali ya ushirikiano katika kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao nchini pamoja na Kutafuta ufumbuzi wa changamoto za serikali mtandao zilizopo nchini ili kuleta  maendeleo ya kiuchumi na kijamii .

Aidha, wataalam wa TEHAMA wa Tanzania wamepata fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalam wengine wanaohusika na Serikali Mtandao kutoka nchi zinazofanya vizuri katika eneo la Serikali mtandao zikiwemo India na Singapore.waliohudhuria Mkutano huo.

Kongamano hilo lenye kaulimbiu “Rasilimali za TEHAMA Zilizowianishwa Zinaboresha Utoaji Huduma Kwa Umma kwa Ufanisi(Towards Harmonized ICT Resources for Effective Public Service Delivery) nichachu kwa maendeleo na litaleta mabadiliko makubwa ya TEHAMA katika taasisi za umma.