Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliandaa Kikao Kazi cha Kwanza cha Serikali Mtandao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (AICC) Jijini Arusha kuanzia tarehe 17 - 20 Agosti, 2015.
Uwianishaji wa Rasilimali za TEHAMA kwa Utoaji Bora wa Huduma kwa Umma
Angalia Nyaraka Angalia ProgramuWashiriki wapatao 786 ambao ni watumishi wa umma kutoka taasisi mbalimbali walihudhuria. Washiriki hao waligawanywa katika makundi mawili: Kundi la kwanza lilifanya kikao tarehe 17 - 18 Agosti, 2015 ambapo Maofisa TEHAMA na Maofisa wanaotumia mifumo ya TEHAMA kutoka Wizara, Idara Zinazojitegemea, Mamlaka, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa walishiriki.
Aidha, kundi la pili lilifanya kikao tarehe 19 - 20 Agosti, 2015 na lilihusisha Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Ni kuweka mazingira bora kwa Wadau wa Serikali Mtandao hususani taasisi za umma kupata taarifa ya mwenendo wa utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao nchini Tanzania na kupata maarifa ya matumizi ya TEHAMA serikalini katika utoaji wa huduma kwa umma na kutatua changamoto za serikali mtandao.