Ufuasi
e-GA inalenga kuboresha uratibu na uwianishaji wa utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma kwa kufanya yafuatayo:
- Uimarishaji wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kwa umma.
- Utoaji wa Viwango na Miongozo mara kwa mara.
- Kujenga uwezo wa taasisi za umma kutumia viwango na miongozo katika hatua za kupanga, kuanzisha na kutekeleza jitihada za serikali mtandao.