Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Mb), leo Desemba 03, 2024 ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), lilolopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mhe.Simbachawene amemtaka mkandarasi Suma JKT na msimamizi wa ujenzi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Nchini (TBA), kuongeza kasi ili kukamilisha jengo hilo mapema mwakani.