emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

WARSHA YA BLOCKCHAIN NA SARAFU MTANDAO (Techcon Tanzania 2024) YAANZA JIJINI DAR ES SALAAM


WARSHA YA BLOCKCHAIN NA SARAFU MTANDAO (Techcon Tanzania 2024) YAANZA  JIJINI DAR ES SALAAM


Warsha ya siku mbili ya kujadili matumizi na umuhimu wa teknolojia ya ‘Blockchain’ pamoja na Sarafu Mtandao (Techcon Tanzania 2024) imeanza leo katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kwa kushirikiana na Chama cha Umoja wa Blockchain Afrika (UABA) ambapo taasisi mbalimbali za umma na binafsi zikiwemo benki, zinashiriki katika warsha hiyo.