emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

KAMATI BARAZA LA WAWAKILISHI YAIPONGEZA e-GA KUTUMIA WATAALAMU WA NDANI UJENZI NA USANIFU MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI.


KAMATI BARAZA LA WAWAKILISHI YAIPONGEZA e-GA KUTUMIA WATAALAMU WA NDANI  UJENZI NA USANIFU  MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI.


Kamati Baraza la Wawakilishi ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC), imeiopongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kwa kutumia wataalamu wa ndani katika ujenzi na usanifu wa mifumo ya TEHAMA Serikalini.

Pongezi hizo zimetolewa hii leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh.Juma Ali Khatib, baada ya kupokea wasilisho kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mhandisi Benedict Ndomba, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya e-GA katika kusimami, kuratibu na kukuza jitihada za Serikali Mtandao nchini.

"Tumesikia kwamba mnatumia vijana wa kitanzania kutengeneza mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayotumika Serikalini lakini pia, mnaendesha kituo cha ubunifu na tafiti ili kukuza na kuibua vipaji vya vijana wengi wazawa, hilo ni jambo zuri kwa usalama wa mifumo yenyewe na usalama wa taarifa za serikali kutokuvuja kwa watu wasiohusika", Amesema Mh.Khatib.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi chini ya Dkt.Hussein Mwinyi, imedhamiria kuleta mageuzi ya TEHAMA hivyo, ameitaka e-GA kuboresha ushirikiano na Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar (eGAZ), ili kutimiza malengo hayo ya Serikali.

Kamati hiyo imefanya ziara katika Makao Makuu ya Mamlaka ya e-GA jijini Dodoma , ili kujionea shughuli za Mamlaka hiyo.