Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Washiriki wa Mkutano wa Serikali Mtandao 2019

Washiriki wa Mkutano wa Serikali Mtandao 2019

Mkutano utakuwa wa Awamu Tatu:

Awamu ya kwanza itakuwa ya muda wa siku mbili, tarehe 30 na 31 Januari, 2019 na kuwashirikisha Wakurugenzi wa TEHAMA, Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini, Maofisa Waandamizi wa TEHAMA, Maofisa TEHAMA na Watumiaji wa Mifumo hususani Maofisa Ununuzi, Maofisa Mawasiliano Serikalini, Maofisa Utumishi, Maofisa Utawala na Maofisa Biashara.

 

Awamu ya Pili itakuwa tarehe 1 Februari, 2019 na kuwashirikisha Maofisa Masuuli wa Serikali Kuu na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

 

Awamu ya Tatu ni tarehe 2 Februari, 2019 na itahusisha washiriki wote waliojisajili kwa ajili ya Siku ya Utafiti na Ubunifu ya Serikali Mtandao.