Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Tunafanya nini

Tunafanya nini

Ili kutimiza Dira na Dhamira yake, Wakala ya Serikali Mtandao ina malengo sita, ambayo  yakitimizwa yataiwezesha kutimiza masharti ya huduma ya wadau na wateja wake.  Malengo hayo ni:-

Kuboresha uwezo wa Taasisi za Serikali kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao;

Wakala inaendesha mafunzo mbalimbali na kuzishauri na kuzisaidia taasisi mbalimbali za umma kujenga uwezo wa watumishi wake katika kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao.

Kuboresha upataji wa huduma mtandao kwa umma;

Wakala ya Serikali Mtandao inaimarisha miundombinu ya msingi kwa ajili ya utoaji wa huduma za mtandao kwa umma na kwa wakati, uwazi, urahisi na gharama nafuu. Wakala imetengeneza mifumo ifuatayo; Tovuti Kuu ya Serikali (www.tanzania.go.tz) ambayo ni dirisha moja la kutolea huduma kwa umma, Tovuti Kuu ya Ajira ambayo inatoa taarifa kuhusu nafasi zote za kazi zinazotangazwa Serikalini na Mfumo wa huduma za Serikali kupitia simu za Mkononi *152*00#

Kuboresha mifumo shirikishi ya TEHAMA

Wakala inaweka mazingira yanayowezesha taasisi za umma kushirikiana katika matumizi ya rasilimali za TEHAMA ili kuondoa urudufu, kupunguza gharama na kuongeza ubora wa huduma kwa umma kwa kufanya yafuatayo; Imesanifu ujenzi wa kituo kidogo cha kuhifadhi na kuendesha mifumo mbalimbali ya Serikali mtandao, imetengeneza mfumo wa barua pepe wa Serikali, inaunganisha taasisi zote za umma katika mtandao mmoja wa mawasiliano.

Kuimarisha uratibu, usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya Serikali Mtandao katika utoaji wa huduma kwa umma;

Wakala inasimamia udhibiti wa viwango vya Serikali Mtandao kwa kutumia miongozo mbalimbali na viwango vilivyowekwa ili kuwa na mifumo bora ya TEHAMA.

Kuboresha huduma za ushauri wa kitaaluma;

Wakala ya Serikali Mtandao inatoa huduma za ushauri wa kitalaamu na msaada wa kiufundi  kwa taasisi za umma. Miongoni mwa misaada hiyo ni kusanifu, kutengeneza na kuendesha Mifumo na tovuti.