Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

MDAs zaaswa kushirikiana na Wakala

MDAs zaaswa kushirikiana na Wakala

2015-03-16

Mkurugenzi wa Miundombinu na Uendeshaji (DCIO) Bw. Benjamin Dotto amewataka Maofisa TEHAMA (Technical Staff) kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali- MDAs kushiriki kikamilifu mafunzo  mbalimbali yanayoandaliwa na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) ili kuwajengea uwezo katika utendaji kazi.

Aliyasema hayo alipokuwa anafunga mafunzo ya “cyberoam” kwa kundi la pili lenye washiriki 36 yaliyoanza Machi 16-18, 2015 katika Hoteli ya Belinda Oceanic Resort.

“Wakala itaandaa awamu ya tatu (3) ya mafunzo ya vifaa vya “Cisco”, “cyberoam” na “power” kwa ajili ya Maofisa TEHAMA wa Serikali, hivyo bado tunahitaji ushiriki wenu”. Alisema Bw. Dotto.

Naye mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka kampuni ya “s. Saidi Buhero ameishauri Wakala kuandaa mafunzo mara kwa mara ili kuwawezesha maofisa TEHAMA Serikalini kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia.

Vilevile, mshiriki kutoka Wakala ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bi. Joan Rwegalulira amesema mafunzo hayo yamempa ufahamu wa mambo mengi kama vile mabadiliko ya teknolojia na umuhimu wake, usalama wa TEHAMA na jinsi ya kumudu kazi zake.

“Mafunzo haya yanatija kubwa kwangu na Serikali kwa jumla kwa sababu ujuzi huu niliopata utanisaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi” Alisema Bi. Rwegalulira.

Mafunzo hayo yalifunguliwa Machi 9 na kufungwa Machi 18, 2015 na yaliwahusisha Maofisa TEHAMA wa Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali 72.