Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Ziara ya Katibu Mkuu OR-MUU katika Ofisi za eGA

Ziara ya Katibu Mkuu OR-MUU katika Ofisi za eGA

2015-02-10

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wakala ya Serikali Mtandao ili kuboresha huduma na kusaidia kukuza jitihada zinazofanywa na Serikali Mtandao.

Amesema hayo katika ziara yake aliyofanya katika Ofisi ya Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo  Jengo la TTCL  mtaa wa samora jijini Dar es salaam Februari 9, 2015.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Hab Mkwizu, aliyeambatana na Katibu Mkuu pamoja na menejimenti ya Utumishi wa Umma ameshauri Wakala kujitangaza zaidi ili jamii ipatae kujua huduma zake na shughuli inazozifanya katika kuboresha huduma zinzaotolewa na Serikali kwa njia ya mtandao.

“Ninawashauri mjitangaze kwenye vyombo vya Habari ili jamii iwafahamu na kutambua huduma zote mnazozitoa pamoja na jitihada zote za Serikali Mtandao katika kukuza teknolojia ya Habari na Mawasilano” Alisema Bw. Mkwizu.