Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Tume Yapata chombo cha Mawasiliano kwa Umma

Tume Yapata chombo cha Mawasiliano kwa Umma

2018-06-08

‘Nimatumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa na manufaa makubwa kwetu na kwa wateja wetu kwa jumla kwa kuwa tovuti ni chombo muhimu sana cha mawasiliano katika dunia ya sasa. Sisi hatukuwa na tovuti lakini kwa hatua hii sasa wananchi watarajie kupata taarifa za umwagiliaji kwa wakati”

 mafunzo ya kupandisha taarifa kwenye tovuti ya Tume yaliayoanza tarehe 5 hadi 8 Juni 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Wakala.

Bw. Fimbo ambaye pia ameshiriki mafunzo hayo kwa lengo la kupata uelewa wa mambo ambayo watumishi wake wanafanya katika tovuti, amesisitiza kuwa, utawala umeona ni vyema kujua mambo wanayofanya watumishi wake ili kurahisisha upangaji wa vipaumbele katika sehemu ya mafunzo kazini.

Naye Bw. Nickson Mashafi ambaye ni Mhandisi Umwagiliaji wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ameomba mafunzo haya kuwa endelevu kwa kuwa teknolojia inabadilika mara kwa mara na hivyo kuwa na elimu inayoenda sambamba na mazingira.

“Binafsi nimefurahi kupata tovuti ambayo ni rahisi sana kutumia hata kama sina elimu ya Tehama. Tovuti hii nimefundishwa na kutambua kuwa naweza kuweka taarifa zozote nikiwa mahali popote palipo na mtandao ni kitu kizurdi na cha kujivunia kama Taifa” ameongeza Bw. Mashafi.

Maofisa wengine wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliohudhuria mafunzo hayo ni Bw. Remigius Rushomesa ambaye ni Afisa kilimo Msaidizi Mwandamizi (PAFO) Nyamhanga J. Chacha-Mhandsi Kilimo (AGE) na Bi. Hamida M. Juma-Mtakwimu na Evelyn Mkokoi-Afisa Habari.