Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika amewataka watumishi wa eGA kufanya kazi kwa weledi na umoja

Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika amewataka watumishi wa eGA kufanya kazi kwa weledi na umoja

2017-10-17

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb), amewataka watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA)  kufanya kazi kwa weledi mkubwa na umoja ili kuhakikisha shughuli za utoaji huduma kwa umma zinakuwa za ubora ili kupunguza gharama na mianya ya rushwa.

Amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Wakala zilizopo jijini Dar es Salaam, Oktoba 17, 2017 na kufanya kikao cha pamoja na watumishi wote wa Wakala hiyo.

“Nimefurahishwa sana na utendaji kazi wenu na moyo wa kujituma kwani kazi iliyofanyika ni kubwa na inaonekana japo ni ndani muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwa wakala hii. Mafanikio haya yanaleta mwanya wa kuona changamoto nyingine ambazo tunatakiwa kukabiliana nazo ili kuhakikisha huduma Serikalini zinapatikna kwa njia ya mtandao” alisema Mhe. Mkuchika

Ziara hii ni mahususi kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizochini ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo yeye ndiye waziri mwenye dhamana, baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mnamo tarehe Oktoba 7, 2017 na kuapishwa Oktoba 9, 2017 kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora