Mamlaka ya Serikali Mtandao ilianzisha Mtandao wa Mawasiliano Serikalini (GovNet) ambao ni salama, rahisi na wenye kuaminika kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano ndani ya Serikali. Kutokana na jitihada hizo, Wizara, Idara na Wakala 72, Mamlaka za Serikali za Mitaa 77 katika mikoa 20 ya Tanzania Bara na taasisi za umma 18 zilizopo mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma zimeunganishwa kwenye mtandao huo. Nyingi...
Inaipunguzia Serikali gharama ya mawasiliano
Inaboresha mawasiliano ya kielektroni mathalani data, sauti na video.
Inaongeza kasi ya intaneti
Inawezesha kutumia mifumo shirikishi ya TEHAMA
Inaongeza ufanisi wa kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma
Taasisi za umma zinaweza kuwasiliana kwa simu za mezani kama vile zimeunganishwa katika jengo moja.
Simu za IP zinaweza kutumika kufanya vikao kwa taasisi za umma
Mtandao shirikishi, salama na wa gharama nafuu katika utendaji na utoaji wa huduma kwa ufanisi