Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Ujumbe wa Mtendaji Mkuu

Kwa niaba ya watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao Tanzania, ninayo furaha kukukaribisha katika tovuti hii ambako  tunatumaini utapata taarifa za kuaminika unazozihitaji kwa ukamilifu kuhusu wigo, upeo wa mamlaka, dira, dhamira, maadili, malengo, mikakati, shughuli kuu, ahadi na maadili  ya Wakala.

Uzinduzi wa tovuti yetu mpya ni tukio la kihistoria katika kufikia dira na matarajio yetu ya kutambuliwa kama taasisi inayoongoza kwa ubunifu, inayowezesha matumizi ya TEHAMA kwa kuboresha utoaji wa huduma kwa umma unaofanywa na Wizara, Idara, Wakala, Mamlaka na Serikali za Mitaa hapa nchini Tanzania.

Kama taasisi mpya, tunajitahidi kudumisha na kutumia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Serikali Mtandao kwenye Kurugenzi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma iliyokuwa na wajibu wa kusimamia na kuratibu jitihada za Serikali Mtandao kabla ya kuanzishwa kwa Wakala.

Lengo letu ni kukabiliana na hali halisi kama ilivyo, kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano na Wizara, Idara, Wakala, Mamlaka na Serikali za Mitaa na wadau wengine katika kutafuta ufumbuzi na njia za kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi kwa kutumia uwezo wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Aidha, kupitia kwenye tovuti hii, utabaini mikakati mbalmbali inayotafsiri dhamira yetu katika uhalisia. Pia kadri muda unavyokwenda, tovuti itaeleza kila hatua thabiti na juhudi zinazochukuliwa na eGA katika kutimiza malengo kama yanavyotafsiriwa kwenye Mpango Mkakati wa Miaka mitano (2012/13  hadi 2016/17). Malengo hayo ni pamoja na kuboresha uwezo wa Wizara, Idara, Wakala na Serikali Za Mitaa kutekeleza jitihada za serikali mtandao; kuboresha upatikanaji wa huduma mtandao kwa umma; kuboresha utumiaji wa pamoja wa nyenzo na miundombinu ya TEHAMA katika kutoa huduma kwa umma; ushauri wa serikali mtandao; kuboresha msaada wa kiufundi, huduma na ushauri wa kitaalamu; kuboresha uwezo wa wakala kutekeleza jitihada za serikali mtandao.

Tovuti hii inaonyesha ubunifu wa hali ya juu ambao tunaamini kwamba itakuwa rahisi kutumia na kupata taarifa kwa  wanaoitembelea. Nimatumaini yangu kuwa kila atayetembelea tovuti hii atapata jambo la kumfurahisha na atarudi mara kwa mara ili tuendelee kuwa na mawasiliano.

Ni nia yetu kuendelea kuboresha tovuti hii kadri muda unavyokwenda ili ipatikane kwa urahisi na ubora wa hali ya juu Tunafurahi sana kuzungumza na watembeleaji wa tovuti waliohamasika na tunathamini  kila maoni tutakayoyapokea.

Nimatumaini yangu kuwa utakuwa umefarijika na naamini muda wako utakuwa umetumika kwa manufaa unapotembelea tovuti yetu.

 


Mtendaji Mkuu,
Wakala ya Serikali Mtandao.