Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Nifanyeje...

Nifanyeje...

Kujisajili na Huduma ya ujumbe mfupi wa Maandishi(sms)

Huduma hii inaiwezesha taasisi za Serikali kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa wananchi.

Masharti:

1. Iwe taasisi ya Serikali.

2. Iwe imejisajili mtandaoni.

Taratibu:

1. Jisajili mtandaoni kwa anuani http://govsms.ega.go.tz/registration form

2.  Lipia idadi ya ujumbe kulingana na mahitaji ya taasisi yako kwa njia ya benki kupitia Akaunti ya Mapato ya Wakala (e- Government Agency Revenue A/C) Na. 20110002340, NMB Bank.

3. Weka taarifa ya malipo kwa kujaza fomu kwa njia ya mtandao.

4.  Utapokea ujumbe wa huduma uliyoomba.